6 Hadithia Kisanii

Richmond Embeywa and Chantelle Warner



Photo: Solomon Kiruri - Kirurisuleiman on Instagram

Kiwango: 

Ya kati hadi ya juu

Maneno makuu: 

hadithi ⧫ wakati uliopita ⧫ vivumishi ⧫ vielezi ⧫ hisia ⧫ mpangilio ⧫ tabia

Summary:

The original lesson was adapted in part from the Narrative Storyboard and activities created around Käthe Kollwitz’s image Weberzug, both developed as part of the Art/Write project. This lesson uses a contemporary image of the Nairobi city market posted on Instagram by a Kenyan Swahili-speaking artist.By focusing attention on the events, but also the mood and relationships, the lesson pushes students to consider how storytelling – in image or text – can not communicate a series of events but also evoke feelings, through the use of verbs, adjectives, and adverbs.

The activity was designed to be done in the gallery, but could also be adapted in the classroom by posting images on the walls and creating a makeshift gallery, or even for online teaching, by providing digitally-mediated images.

Muhtasari:

Somo la asili liliteuliwa kutoka kwa ubao wa hadithi pamoja na zoezi zilizoshirikisha picha ya Weberzug ya msanii Käthe Kollwitz, zoezi ambazo zilianza kama mradi wa Art/Write (Sanaa/Kuandika). Somo hili linatumia picha iliyowekwa kwenye Instagram na mkenya ambaye ni mzungumzaji wa Kiswahili kuonyesha soko la jiji la Nairobi. Kwa kuangazia matukio, lakini pia mhemko na mahusiano, somo linawalazimu wanafunzi kufikiria ni vipi hadithi – picha au maandishi – zinavyoweza/ au kutoweza pasha Habari matukio ila pia kuamsha hisia kupita vitenzi, vivumishi na vielezi.

Zoezi hili lilikusudiwa kufanyika kwenye maonyesho lakini pia linaweza kufanyika darasani kwa kutundika picha kwenye kuta kama meonyesho ya muda mfupi, na pia kwa kufunza mtandaoni, kwa kutoa picha za kidigitali.

Malengo ya somo:

  • Kuweza kusimulia hadithi (kwa usaidizi);
  • Kuweza kusimulia au kuripotia, lile ambalo mtu analopitia, anaona au anafanya na watu wengine;
  • Kuweza (kwa sentensi rahisi zinazohusiana) simulia tajriba, matukio, matumaini na malengo.

Je, hadithi inasimuliwa vipi kutumia picha?

Kupatana na ufafanuzi, hadithi ina fomu mbalimbali. Jambo lazima lifanywe. Hadithi huhusisha matukio kadhaa. Picha ni tuli. Ama? Katika zoezi hili tutafakari jinsi aina mbalimbali za matukio yanayoweza kusimuliwa kupitia picha.

Dokezo: Maswali yafutayo yanaweza jadiliwa kwanza kama kazi ya ziada au kwa ushirikiano na mwenzio au kama kikundi.

  1. Sauti iko vipi?
thabiti sisitizi ya kukataa ya kukosoa fumbo
kejeli Ya kubaliana bila upendeleo kejeli na kadhalika
  1. Je, picha hii ina athari gani kwako?
  2. Je, mpangilio uko vipi? Unahitaji maneno gani kueleza mazingira?
  3. Je, wahusika ni kina nani? Wana miaka mingapi? Ni ishara zipi za uso zimewakilishwa? Wamevaa mavazi gani? Wamekaa vipi? Unadhani wahusika wanajinsia gani? Unadhani wahusika wana tabaka gani?
  4. Je, wahusika wanaingiliana vipi? Uhusiano wao ni upi?
  5. Je, wahusika wanaonyesha hisia zipi? Mbona wafikiri hivyo? Haya yanawezasimulia vipi kwa maonyesho?
  6. Ni jambo gani linafanyika? Haya yamesimuliwa vipi kwa maonyesho?

Hadithi inaweza simuliwa vipi kwa maandiko? 

Andika hadithi mwafaka ya picha hili. Tumia mawazo yako kuhusu sauti, mazingira and wahusika uliyoyatumia katikia zoezi la kwanza. Hadithi inahitaji wahusika pamoja na matukio ambayo hayako kwenye picha.

Tumia bodi ya hadithi iliyo hapa chini kupanga hadithi yako. Ongeza mistari mipya inapohitajika.

 

Picha nyakati simulizi Je, ni jambo gani linafanyika? (Jibu maswali ya kushoto)
Anza na picha Mwelekeo

Nani? Nini? Lini? Wapi?

Eleza kwa mchoro matukio yanayofuata. Tatizo

Na jambo gani limefanyika baadaye?

Eleza kwa mchoro yaliyofanyika mwishoni. Suluhisho

Jambo gani lilifanyika mwishoni?

Hitimisha hadithi yako kutumia mistari 5-7.

Picha moja, maoni tofauti? 

Linganisha hadithi yako na maoni ya wanafunzi wenzako.

Kuna ulinganifu upi? Kuna tofauti gani?

License

Icon for the Creative Commons Attribution 4.0 International License

Multiliteracies at the Museum: A Resource Book for Language Teachers Copyright © 2022 by Chantelle Warner is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License, except where otherwise noted.

Share This Book